![]() |
Seneta wa Bungoma Moses Wetangula, |
Mahakama ya juu imesimamisha kituo
cha BBC kutomhusisha seneta wa Bungoma Moses Wentagula, na madai ya kuhongwa na
kampuni ya sigara ya British American Tobacco
(BAT)
Wetangula kwa ombi lake la dharura, kwa mahakama ya
juu, alisema kuwa kituo hicho kilimharibia jina katika kipindi chao
kijulikanacho kama Panorama, ambacho kinadai kuwa seneta huyo aliomba kukatiwa tikiti ya ndege, kwa niaba
ya mkewe kwenda London kwa njia isiyo wazi.
Kulingana na
senator huyo, kipindi hicho kilitangaza kuwa yeye alihusishwa na ufisadi,
ambapo alishirikiana na kampuni ya BAT na kumhonga wakati alipokuwa akihudumu
kama waziri wa biashara ,katika enzi za rais mstaafu Daniel Arap Moi.
Senator huyo kupitia mshauri wake mkuu ,James Orengo, alisema kuwa taarifa hiyo iliyo peperushwa na BBC, imezidi tutambaa katika mtandao wa kijamii , runinga pamoja na televisheni ,jambo ambalo limesababisha yeye kuchukiwa bure.
No comments:
Post a Comment