Friday, 2 September 2016

HOJA YA KUMUONDOA GAVANA GACHAGUA MAMLAKANI YAPITISHWA.

Gavana Nderitu Gachagua.
Na Mwangi K.Githinji.

Hoja ya kumuondoa mamlakani gavana wa Nyeri Nderitu Gachagua imepitishwa na wawakilishi wa kaunti hiyo.

Kulingana na spika wa bunge hilo Mwangi Mugo ni kuwa hakuna aliyepinga mswada huo kwenye bunge hilo huku wote wakiiunga mkono kwa pamoja.

Amesema kuwa hatua itakayofuata ni kuwasilisha uamuzi huo kwa bunge la seneti ambalo sasa litachukua hatamu kwa kutengeneza kamati  itakayofanya uamuzi kuhusu hatma ya Gachagua.

Wawakilishi hao wanamshtumu gavana huyo kwa kutotii mamlaka ya bunge hilo,Kutumia fedha za kaunti vibaya na kushindwa kwake kupitisha bajeti na vile vile matumizi mabaya ya afisi yake.


Mwanzoni wawakilishi wanaomuunga mkono gavana Gachagua waliondoka katika kikao cha leo baada ya mawakili wake kunyimwa nafasi ya kuhudhuria kikao hicho.

No comments: