Friday, 24 July 2015

HABARI KUU KUHUSU UJIO WA RAIS BARRACK OBAMA




Usalama unazidi kuimarishwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa jomo Kenyatta, kufwatia ziara ya rais wa Marekani Barrack Obama.

Maafisa wa usalama wanashika doria katika uwanja huo kwa lengo la kuimarisha usalama kabla ya kuwasili kwa Raisi Barack Obama mwendo wa saa mbili unusu leo usiku. 

Wanafunzi wa shule ya upili ya Makini wametamatisha maandalizi yao ya  kumtumbwiza rais Obama katika ikulu ya rais hapo kesho.

Baadhi ya barabara atakazo tumia rais Obama zishafungwa ikiwemo ile ya Waiyaki,chiromo na barabara kuu ya kuelekea Mombasa huku barabara kuu ya Thika na ya Limuru zikitarajiwa kufungwa baadae hapo kesho na jumapili.

Hata hivyo nyanyake rais Obama mama Sarah amewasili hapa jijini katika ndege ya shirika la Kenya airways,huku akitarajiwa kukutana na rais Obama pindi tu atakapowasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Wananchi kutoka eneo la Kogelo kaunti ya Siaya watakuwa wakifwatilia matukio ya Rais Obama moja kwa moja kutoka kwenye runinga kubwa zitakazowekwa katikati mwa mji. Hii ni  baada ya kusemekana kuwa  rais Obama hatazuru eneo hilo.

Tutakupasha matukio yote kulingana na ziara hiyo pindi tu yatakapojiri,
Kumbuka unapata matangazo hayo katika steshenu yako nambari moja ya kijamii ECN Radio…

Tuskize kupitia tufuti yetu ya www.mixlr.com/ecn-radio

No comments: