Thursday, 24 November 2016

MIUNGANO MIKUU YA KISIASA NCHINI YAENDELEA KULAUMIANA KUHUSU UFISADI.



Raila Odinga, Agnes Zani na maafisa wengine wa ODM
Raila Mwangi

 Viongozi wa chama cha Jubilee na wale wa mrengo wa ODM, wamerushiana cheche za maneno, baada ya kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale kudai kwamba kinara wa ODM Raila Odinga anawatetea baadhi ya viongozi wa chama chake wanaohusishwa na sakata za ufisadi.

 Hii ni kutokana na kufujwa kwa takriban shilingi milioni hamsini na moja katika kaunti ya Kilifi, inayoongozwa na gavana Amason Kingi kisha Odinga kumtetea Kingi.

 Odinga akiongea katika makao yake makuu yaliyo Capital Hill hapa jijini Nairobi akiwa ameandamana na zaidi ya wabunge kumi wa ODM, Raila alisema kuwa hajajaribu kuwatetea magavana wafisadi katika muungano wa CORD kama ilivyodaiwa na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Aden Duale, akikariri kuwa serikali ya Kilifi ilichukua hatua kwa kuwatimua maafisa fisadi katika kaunti hiyo.

Duale hata hivyo ametetea madai yake huku akisema kuwa ana ushahidi wa kutosha kumhusisha Raila na ufisadi katika kaunti anazoongoza ingawa mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Mombasa Mishi boko amemtetea Odinga.

No comments: