Thursday, 24 November 2016

RAIS KENYATTA AWAJIA JUU WAPINZANI NA KUMTETEA AFISA WAKE.

Rais Kenyatta akiwa anatabasamu
Robert Mwangi.

Rais Uhuru Kenyatta amemtetea mkuu wa utumumishi wa umma Joseph Kinyua kihusiana na madai kuwa aliidhinisha kwa njia isiyo halali malipo ya shilingi milioni mia nne kwa wasambazaji bidhaa katika wizara ya afya.

Akiongea katika eneo la Kandui kaunti ya Bungoma wakati wa mahala ya kwanza ya chuuo kikuu cha Kibaabi rais Kenyatta amesema kuwa waliolipwa walitoa huduma zao kwa wakenya.

Kiongozi wa taifa hata hivyo ametoa wito kwa wakaazi wa Bungoma kuunga mkono serikali ya Jubilee ili kuhakikisha kuwa wanafufua kiwanda cha karatasi kilichosambaratika cha Webuye.


Aidha rais amewataka wapinzani  kukosoa serikali kwa njia inayofaa huku akiwakashifu kwa kueneza propaganga.

No comments: