![]() |
Mchezaji wa Liverpool Mane. |
Na Mwangi K. Githinji.
Sajili mpya wa Liverpool Sadio Mane alipelekwa
hospitalini Kusini mwa Liverpool ili
kufanyiwauchunguzi kwenye bega lake baada ya kupata jeraha akiwa mazoezini.
Inaripotiwa kuwa mchezaji huyo aliondoka Liverpool
akiwa amefungwa mkononi mwake ishara kuwa alikuwa ameumia japo inakisiwa kwamba
jeraha hilo sio mbaya sana.
Katika mechi yao ya mwisho sajili huyo mpya
alionyesha viwango vizuri vya mchezo katika ushindi wao wa mabao 4-3 dhidi ya
arsenal ambapo pia alifunga goli.
Liverpool wanajiandaa kuchuana na Burnely katika
mechi yao ijayo ya ligi.
No comments:
Post a Comment