![]() |
Stephen Soi aliyekuwa mkuu wa Kikosi cha Kenya kilichoshiriki Olimpiki Rio |
Ben Kirui
Aliyekuwa mkuu wa kikosi cha Kenya kilichoshiriki
mashindano ya Olimpiki jijini Rio nchini Brazil Stephen Soi pamoja na maafisa
wengine wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo kujibu mashtaka
mbalimbali kuhusiana na jinsi wanariadha wa Kenya walivyodhalilishwa kule Rio.
Soi ambaye
aliachiliwa huru kwa dhamana ya elfu hamsini, naibu wake James Chacha pamoja na
katibu mkuu wa kamati ya kitaifa ya Olimpiki Nock Paul Francis walikamatwa
ijumaa punde tu walipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA kutoka
Rio na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga.
Haya yanajiri
huku shinikizo za kutaka waziri wa michezo Hassan Wario kujiuzulu zikiendelea
kutokana na usimamizi mbaya wa wanaridha wa Kenya.
No comments:
Post a Comment