![]() |
Kinara wa Cord Raila Odinga akikaribishwa na Rais wa Tanzania John Magufuli |
Ben Kirui
Kinara wa
Cord Raila Odinga amerejea nchini kutoka Tanzania huku mjadala kuhusu sababu
yake ya kususia kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa azma ya Seneta wa Bungoma Moses
Wetangula kugombea kiti cha urais ukishika kasi.
Raila
amekwepa waandishi wa habari punde tu alipowasili nchini kutoka ziara yake ya
siku tatu kwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Kulingana na
wandani wake wa karibu, Raila alibadilisha mipango yake siku ya jumamosi
alipokuwa akielekea Kakamega kwa sababu ya ripoti za kuzuka kwa ghasia katika
bustani ya Muliro Gardens ambapo mkutano wa Wetangula ulikuwa ukifanyika.
No comments:
Post a Comment