By Julius Jumah
Samahani sana wanangu.
Wanangu salamu.
Hizi ni salamu za dhati, za upendo.
Salamu zitokazo ndani na mvunguni mwa moyo wangu.
Salamu zilizobeba dhati ya nafsi yangu.
Salamu adimu kwenye ulimwengu tunamoishi.
Nisameheni wanangu.
 |
Moyo umenituma........ |
Moyo wangu umenituma barua niwaandikie.
Nyie wana na vijana wangu.
Ikikufikia mweleze na mwenzako.
Mmmh mwanangu, niandikapo barua hii,
Najua mko mahala flani.
Ama ni asubuhi jasho likiwatiririka kwa kuangalia
ponografi kwenye intanet kafee baada ya kutoroka shuleni.
Si ajabu kuwa ni usiku wa manane, mmegeuka kuwa bidhaa zinazotembea nusu uchi
mkifukuzana na polisi, rambo mkononi wasijue mmefikaje pale.
Na pengine, licha ya umri wa miaka 12, mko leba
mkisubiri ule wakati mchungu sauti ya muuguzi ikikwambia pipi ulimumunya peke
ako.
Wanangu, pengine ni usiku katikati mko kwenye pati
ya kucheza uchi ujira ni pakiti ya sigara.
Au labda mko shuleni chini ya miti mkisoma, mliopo kwenye vyumba mmejaa mithili
ya siafu.
Yawezekana pia kuwa ninapoandika waraka huu mpo
majalalani mkichakuachakua vifusi vya taka kama kuku wa kienyeji kutafuta
makope ya kuchezea.
Ama mwacheza mpira wa makaratasi vichochoroni maana
uwanja wenu umezungushwa mabati na kuandikwa "mbwa kali" kisha ujenzi
wa kasino.
Walonyakua ardhi yenu ya shule ya Lang’ata bado wapo
mamlakani wakiitwa ‘Private Developer’, walofuja mamilioni yenu zaidi ya mia
saba bado wapo na kupigiwa upato kutwaa ugavana kaunti fulani.
Wanangu lakini pengine mmejikongoja hadi sekondari.
Maisha ya manamba ndio staiki yenu, bila mikiki hakuna lishe.
 |
Uchungu wa mwana aujuae mzazi |
Wanangu, machozi yanitiririka kiwango cha kulowesha
karatasi hii.
Mniruhusu wanangu nkomee hapo, ntaendelea nafsi ikijikubali.
(Asante sana nguli Mrisho
Mpoto)
Ungana nami kwenye:
Facebook: Jumah Mlavidavi
FBPage: Kocha Mlavidavi Jumah
Twitter: @Jumah_Mlavidavi
Instagram: Jumah_Mlavidavi