Saturday, 4 February 2017

MLAVIDAVI CHRONICLES: SURA MBAYA, BEI GHALI

By Julius Jumah
Kitabu kimoja cha shule katika jimbo la Maharashtra nchini India, kimezua ghadhabu baada ya kusema kuwa watu wenye sura mbaya wanastahili kulipa mahari zaidi.
Kitabu hicho kinasema kuwa ikiwa msichana ana sura mbaya au ni mlemavu, inakuwa vigumu kwa wasichana huyo kuolewa na hivyo bwana harusi na familia yake huomba mahari zaidi.
Baadhi ya sura tendeti duniani


Waziri mmoja alivyambia vyombo vya habari kuwa aya hiyo itaondolewa baada ya picha za ujumbe huo kusambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Ulipaji mahari ni tamaduni ya karne nyingi kusini mwa bara Asia, ambapo wazazi wa bibi harusi hutoa pesa, nguo na vito vya thamani kwa familia ya bwana harusi.
Mizozo inaweza kuibuka kuhusu nipesa ngapi zinaweza kulipwa. Wakati mwingine endapo bwana harusi na familia yake hawalipwi, Bi harusi anaweza kudhulumiwa vibaya.

No comments: