By Julius Jumah
Polisi nchini Tanzania inawashikilia zaidi ya watu 10 wakiwemo wasanii maarufu na polisi waliotuhumiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Polisi nchini Tanzania inawashikilia zaidi ya watu 10 wakiwemo wasanii maarufu na polisi waliotuhumiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Miongoni mwa watu hao wanaohojiwa yupo msaani maarufu na miss
Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, aliyeitikia wito wa polisi pamoja wasanii
wenzake kufika kwa mahojiano.
Hapo jana mkuu wa Mkoa huo wa Dar es Salaam, Paul Makonda
aliwataja watuhumiwa kadhaa wakiwemo polisi na wasanii kuhusika na biashara
hiyo na kuwataka leo kuwaripoti kituo cha polisi.
![]() |
Wema Sepetu almaarufu Madam |
Kamanda Sirro amesema kwa sasa imeundwa timu maalum
inayowahusisha polisi na vyombo vingine vya usalama ili kuendelea kuwatafuta
wafanya biashara wa madawa hayo.
Biashara ya madawa ya kulevya ni miongoni mwa matatizo
yanayoikabili nchi ya Tanzania ambapo baadhi wamekuwa wakiinyooshea kidole
serikali kwamba hajaichukua hatua kali ya kukabiliana na tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment