![]() |
vijana wanodaiwa kuwa alshabaab |
Chifu mmoja ameripotiwa kuuwawa kufuatia shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na magaidi wa kundi Al Shabab katika eneo la Omar Jillo huko Mandera.
Kulingana na kamanda wa polisi wa utawala kaunti hiyo Suleiman Hussein, magaidi hao walivamia nyumba ya chifu huyo saa nne usiku wa
kuamkia leo na kumuua kwa kumpiga risasi.
Aidha wahalifu hao wanaarifiwa kuwateka nyara
polisi wawili wa akiba huku ripoti ikiarifu kuwa wamevuka nao na kuelekea katika taifa jirani la Somalia.
No comments:
Post a Comment