Wednesday, 23 December 2015

MAGUFULI TENA AFUNGA KUFURI ZA UFISADI, KUNANI?

NA JULIUS KARIITHI

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi afisa mkuu wa reli, na kuagiza upelelezi kufanywa mara moja kuhusiana na madai ya utoaji wa zabuni katika mchakato wa kuundwa kwa reli ya kisasa maarufu kama  Standard Gauge Railway.
Taifa la Tanzania lilisema mnamo Machi kuwa, mpango wake wa kutumia Dolar billion 14.2 kukarabati reli hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, na kuwa itafadhiliwa kwa mikopo ya biashara wakati taifa hilo linapania kuwa kitovu cha ukanda wa usafiri.
Magufuli alisema kuwa kuachishwa kazi kwa Benhadard Tito ,aliye mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Reli Assets Holdings (RAHCO), kutasafisha njia ya uchunguzi kabambe wa ukiukaji mkubwa wa taratibu za ununuzi, ili kuwezesha kuendelea kwa ukarabati huo.
Rais huyo aliyechukua uongozi mwezi uliopita ameapa kuwang’oa wafisadi wote ndani ya taifa hilo na tayari amekwisha wafuta kazi baadhi ya maafisa wakuu serikalini.