![]() |
| Mtihani wa mwaka huu unafanywa chini ya uangalifu mkali kuzuia udanganyifu kama ulivyoshuhudiwa mwaka jana |
Racheal Kithaka
Mwanafunzi wa kidato cha nne amefariki huko Nakuru
muda mfupi kabla ya kuanza kwa mtihani wa KCSE mapema leo.
Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Nakuru Ester Muiru
amedhibitisha kifo cha mwanafunzi huyo Francis Gikonyo wa shule ya upili ya
Jomo Kenyatta eneo la Bahati.
Muiru anasema mwanafunzi huyo aliugua muda mrefu na
akafariki akipokea matibabu hospitalini.

No comments:
Post a Comment