![]() |
| Ngilu asemezana na Kalonzo |
Robert Mwangi
Kiongozi wa chama cha NARC Charity Ngilu amesema kuwa
serikali ya Jubilee imeshindwa kutimiza ahadi zake huku uchaguzi mkuu ukuzidi
kubisha hodi.
Ngilu amesema kuwa mkataba wiliotia kati ya chama chake cha
NARC na muungano wa Jubilee uliojumuisha TNA na URP umekiukwa.
Ngilu aidha amesema kuwa mkataba huo uliojumuisha hoja tano
zikiwemo haki ya maji kwa kila mkenya, afya na kuinua nafasi ya kina mama,
umekosa kutiliwa maanani na viongozi wa Jubilee.
Suala la iwapo Ngilu atajiunga na muungano wa CORD limesalia
kitendawili licha ya yake kigogo huyo wa chama cha NARC kuonyesha ishara ya
kutaka kufanya kazi na vinara wa muungano wa CORD.

No comments:
Post a Comment