![]() |
| Mwili wa refarii aliyepigwa kichwani na mchezaji mmoja nchini Mexico |
KAPEDO JNR
Polisi nchini Mexico wanamsaka mchezaji mmoja wa
kandanda anayetuhumiwa kwa kumpiga kichwani refarii wa mechi iliyogaragazwa
uwanjani Amigos del Balon mnamo tarehe 6 Novemba 2016, baada ya kuonyeshwa kadi
nyekundu.
Mashabiki waliokua uwanjani walidhani muamuzi wa
katikati mwa uwanja alikua amepoteza fahamu, baada ya kugongwa kichwani kwenye tendo
hilo la unyama
Juhudi za Wafanyikazi wa Shirika la msalaba mwekundu
kujaribu kumuokoa muamuzi huyo hazikufua dafu, baada ya kugundua alikuwa
amepoteza uhai wake.
Mchezaji huyo aliingia mafichoni baada ya tukio hilo
kwa kutumia gari aina ya Pick-up, wakati refarii alikua akipata matibabu.
Refarii huyo kwa jina Victor Trejo kutoka nchini Mexico
alipigwa na mchezaji huyo ambaye alikuwa amepandwa na hasira baada ya kulishwa
kadi nyekundu
Tukio hilo lilitokea jumaapili ya tarehe sita mwezi
Novemba mwaka elfu mbili kumi na sita, katika uwanja mmoja kwa jina la
kihispaniola “Amigos del Balon” utafsiri wake ukiwa “marafiki wa mpira” ambao
unapatikana kule Tulancingo nchini Mexico.

No comments:
Post a Comment