
KAPEDO JNR
Cristiano Ronaldo amesema kuwa
ataendelea kuchezea miamba wa Uhispania Real Madrid kwa muda wa miaka kumi
baada ya kuongeza kandarasi yake uwanjani Santiago Bernabeu
Kandarasi ya mshambulizi huyo
mwenye umri wa miaka 31, ilitarajiwa kukamilika mwezi Juni 2018, lakini
ameiongeza kwa miaka kumi zaidi hadi Juni 2021.
Mshambulizi huyo ambaye zamani
alikuwa akichezea Manchester United, amesema kuwa nia yake ni kukamilisha miaka
yake ya kucheza kwenye Ulingo wa Soka
Kwa upande wake rais wa klabu
hio Florentino Perez, amesema kwamba anampigia upato Mreno huyo kusalia
uwanjaniBernabeu kwa miaka mingi ijayo.
Ronaldo amefungia Real Madrid
mabao 371 tangu ajiunge na klabu hio kutoka Manchester United mwaka 2009 na
amesaidia klabu hio kutwaa taji la klabu bingwa barani ulaya mara mbili na pia
kuiwezesha Madrid kushinda taji la ligi kuu ya Uhispania La Liga.
No comments:
Post a Comment