Tuesday, 8 November 2016

MUUAJI ASIYETAMBULIKA AWAUA MASHABIKI 9 WA SOKA SUDAN KUSINI

KAPEDO JNR

Watu tisa wameuawa na wengine kumi na moja kujeruhiwa katika mji mkuu wa Sudan kusini, baada ya kushambuliwa na mtu asiyejulikana

Polisi mjini Juba wamedhibitisha kisa hicho wakisema kuwa mtu huyo ambaye alikua amefunika uso wake aliwafyatulia risasi watu ambao walikua wanatazama mechi ya Soka katika runinga wikendi iliyopita

Lengo la shambulizi hilo ambalo lilitokea usiku wa jumaamosi kule kusini magharibi mwa mji wa Gure hailikueleweka

Taifa la Sudan Kusini limekumbwa na visa vya mashambulizi tangu vita vikuu vilivyozuka mwezi Disemba 2013

Msemaji wa polisi Sudan Kusini Daniel Justin, amesema kuwa Uchunguzi unaendelea huku akidhibitisha kuwa watu sita waliuawa katika kisa hicho na wengine watatu wakaaga walipokua wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu, vita vimekua vikizuka mjini Juba tangu Julai mwaka huu.



No comments: