Thursday, 10 November 2016

MCHEZAJI BORA WIKI HII: PIERRE EMERICK ABUMEYANG’


Picha: Pierre Emerick Abumeyang'
KAPEDO JNR

Pierre Emerick Abumeyang ameibuka kuwa mchezaji bora wiki hii, baada ya kutia kimyani mabao manne dhidi ya Humburg mnamo tarehe 5 Novemba 2016, katika mechi ya kuwania taji la ligi kuu ya Ujerumani kwenye uwanja wao wa nyumbani, mechi ambayo Dortmund ilishinda 5- 2


Abumeyang’ ambaye alizaliwa tarehe 10 Juni 1989, kule LAVAL nchini Ufaransa, ni mshambulizi ambaye huchezea timu ya taifa ya Gabon, na pia huchezea klabu ya Borussia Dortmund ambayo inashiriki katika ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga

Abumeyang’ anajulikana kwa mwendo wake wa kasi na ubunifu uwanjani, huku akiandikisha rekodi ya kukimbia mita 30 kwa muda wa sekunde 3.7, jambo linalomfanya kuwanyanyasa na kuwaacha hoi mabeki wa klabu pinzani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na saba, alianza taaluma yake katika klabu ya AC Millan kule nchini Italia.

Kwenye msimu wa elfu mbili na nane Ac Millan ilimwachilia kwa mkopo kwenda klabu ya Dijon kule nchini Ufaransa, ambako alifungia timu hio mabao 10
Mnamo tarehe 24 Juni 2009, klabu ya Lille ilitangaza kumsajili mshambulizi huyo kwa mkopo, lakini baada ya fomu yake kudorora walimtuma kwenda kwa mahasimu wao FC Monaco.

Kwenye msimu wa 2012- 13, Abumeyang’ alimaliza wa pili katika mashindano ya kuwania mchezaji bora msimu huo, baada ya kufunga mabao 19 chini ya Zlatan Ibrahimovic
Ni katika msimu huo ambapo Abumeyang’ alishinda taji la Mchezaji Bora Barani Afrika
Mnamo tarehe 4 Julai 2013, Abumeyan’ alijiunga na miamba wa Ujerumani Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka 5

Aidha, Abumeyang’ alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na klabu ya Dortmund dhidi ya mahasimu wao Bayern Munich, kwenye mechi ya kuwania Kombe la DFL Super Cup, mechi ambayo Dortmund ilishinda kwa mabao 4- 2

Mnamo tarehe 31 Julai 2015, Abumeyang’ aliongeza mkataba kwenye klabu hio hadi mwaka wa 2022

Katika msimu wa 2015-16, Abumeyang’ aliifungia Dortmund mabao 25, huku akimaliza wa pili chini ya Robert Lewandoski wa Bayern Munich’, msimu ambao Abumeyang’ alitajwa kua Mchezaji Bora kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga

No comments: