By Dennis Milimo
![]() |
Mmoja wa jamaa waliokuwa katika kituo cha mabasi mjini mombasa akipiga picha na mbwaa anayedaiwa kuwa abiria lakini akagiuka na kuwa mbwa. |
Kioja
kilizuka katika kituo cha mabasi mjini Mombasa, baada ya madai kuwa abiria
mmoja aliyekuwa akisafiri kutoka Kitui kuelekea Mombasa aligeuka kuwa mbwa,
punde tu alipokuwa akishuka basi hilo. Jamaa waliokuwa kwenye kituo hicho cha
basi walieelezea mshangao wao, huku jibwa hilo likifululiza kwenye duka moja na
kujilaza.
Wakaazi
hayo walielezea kwa mshamngao tukio hilo ambali lilikuwa la kishitua sana
miongoni mwao.
Wengi wa
waliokuwa katika kituo hicho cha mabasi walimtizama mbwa huyo aliyekuwa
amejizala njee ya duka moja , huku mwenye duka akishindawa kumtimua kwa hofu
kuwa huenda akagiuka tena na kuwa binadamu.
Baadhi ya
watu waliokuwa katika kitu hicho cha mabasi walimchangamkia mbwa huyo ma hata
kupiga picha naye wasijali maajabu yaliyoandamana naye.
Watu wa
kitui wanajulikana sana kwa mazingaombwe
maarufu kama “kamote” ambayo hutumika kwa njia mbali mbali katika neo
hilo. Hii ni sababu moj aliyofanya watu kuamini kuwa mbwa huyo alibadilika
kutoka abiria hadi mnyama wa miguu mnne.
Inadaiwa
kuwa mbwa huyo alijilaza katika duka hilo kwa muda kabla ya kuondoka na kwenda
zake ,wenyeji wasijue alikoelekea.
Mji wa Mombasa
umehusishwa na uwepo wa majini pamoja na mazingaombwe. Lakini kumbuka
ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.
No comments:
Post a Comment