Friday, 1 April 2016

KWS KUWEKA UA KUZUIA WANYAMA PORI DHIDI YA KUTOKA

Mkurugenzi wa KWS Kitili Mbathi
Ben kirui

Mkurugenzi wa shirika la uhifadhi wa wanyamapori nchini KWS Kitili Mbathi anasema wanalenga kuweka ua litakalosaidia kuzuia wanyama pori dhidi ya kutoka nje punde ujenzi wa barabara ya mkato  itakapokamilika.
Mbathi anasema ujenzi wa barabara hiyo inayopitia katika mbuga ya wanyamapori hapa Nairobi umeathiri pakubwa shughuli katika mbuga hiyo.
Akizungumza katika makao makuu ya KWS Mbathi aidha ametetea hatua ya maafisa wa shirika hilo kumuua kwa kumpiga risasi simba siku ya jumatano katika eneo la Isinya.


No comments: