![]() |
Polisi wanachunguza kisa cha mwanamme kumuua mkewe |
Ben Kirui
Polisi eneo la Koibatek kaunti ya Eldama Ravin wanachunguza
kisa ambapo mwanaume mmoja amemuua mkewe na kisha kumteketeza mwanawe.
Kulingana na polisi na wenyeji wa kijiji cha Moringwo,
mwanamme huyo Moses Keitany alimgonga mkewe kwa kichwa mara kadhaa akitumia
chuma akimuua papo hapo.
Walioshuhudia kisa hicho wamesema kuwa mwanamme huyo
alimchukua mwanawe wa miaka saba baada ya kutekeleza unyama huo na kujifungia
kwa nyumba kabla ya kuiteketeza.
Hata hivyo, waliokolewa na majirani na kukimbizwa katika hospitali
kuu ya Rift Valley.
No comments:
Post a Comment