Wachezaji wawili wa Gor Mahia, Michael Olunga na Karim Nizigiyimana wametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huu.
![]() |
Mshambulizi wa Gor, Michael Olunga. |
Bernard Mang’oli wa AFC Leopards na mshambulizi wa Tusker Jesse Were pia wanawania tuzo hiyo ya dhamana ya shilingi milioni moja.
Katika kitengo cha mkufunzi bora, Frank Nuttal wa Gor, Paul Nkata wa Tusker, Robbert Matano wa Ulinzi na Twahir Muhiddin wa Bandari wote wametajwa kuwania tuzo hiyo.
Kipa bora atakuwa anawania Boniface Oluoch (Gor Mahia), Jairus Adira (Chemelil Sugar), Faruk Shikhalo (Muhoroni Youth), Wilson Obungu (Bandari)
Mlinzi bora wa mwaka huenda akawa Karim Nizigiyimana (Gor Mahia), Noah Abich (Mathare United), Shariff Mohammed (Bandari), Geoffrey Kokoyo (Ulinzi Stars), Musa Mohammed (Gor Mahia)
Tuzo ya Kiungo bora wako wachezaji wanne ambao ni Khalid Kaucho, Eric Johanna, David Kingatua, na Anthony Kimani.
Kisha mchezaji mpya wa mwaka wanawania Ebrimah Sanneh (City Stars), Eston Esiye (Western Stima), George Mandela (Muhoroni Youth), Alphonce Ndonye (Mathare United), Luis Masika (City Stars)
No comments:
Post a Comment