![]() |
Kisiwa cha migingo |
Ben Kirui
Huenda mzozo
baina ya Kenya na Uganda ukatatuliwa wakati ambapo maafisa wa nchi zote mbili
watakutana kwa majadiliano wiki ijayo.
Kamishna wa
eneo la Nyanza Wilson Njenga amesema vikundi hivyo viwili vya maafisa wa
usalama vitakutana kampala Uganda jumatano ijayo.
Njenga amekariri
kuwa mzozo huo ni suala kati ya mataifa mawili na mapatano kati ya serikali
zote mbili yatasaidia sana kufanikisha suluhu kuhusu umiliki wa kisiwa hicho.
Kisiwa cha
Migingo kimekuwa kikizozaniwa na Kenya na Uganda kwa miaka kadhaa.
1 comment:
Migingo belongs to kenya. Period!
Post a Comment