Friday, 8 April 2016

AFUNGWA MAISHA KWA SHTAKA LA UNAJISI

Mwanaume ahukumiwa na mahakama ya kibera kwa madai ya unajisi
Ben Kirui

Mahakama ya Kibera imemhukumu mwanamme mmoja kifungo cha maisha gerezani kwa shtaka la unajisi.
Joseph Muli ameshtakiwa kwa madai ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka sita eneo la Kibera mwaka jana. Mtoto huyo anadaiwa kushawishiwa na peremende kabla ya kuingia katika Nyumba ya mzee huyo aliyembaka.

Mshukiwa ana muda wa majuma mawili kukata rufaa.

No comments: