![]() |
Mfano wa sanduku la kuzika marehemu akiwa angali ameketi, kama ilivyotumika katika mazishi ya Bungoma. |
Wenyeji wa kijiji cha Mungore kaunti ya Bungoma walimiminika kwa makumi kushuhudia maziko ya
ajabu, ya jamaa mmoja ambaye kulingana na amri ya koti alizikwa akiwa ameketi
chini.
Mwenda zake Chrisantus Rapong’o aliyekuwa na umri wa
miaka 75, alifuata njia ya marahaba mnamo Septemba na bila kupusa wazee wa
kanisa alilokuwa akishiriki wakaaza matayarisho kabambe ya kumpumzisha.
Hata hivyo shughuli yenyewe ilionekana kutatizwa na
itikadi za tamaduni yake, wakati jamaa yake ilisisitiza kuwa kulingana na
tamaduni ya Abakhibe, wanaume wanastahili kuzikwa wakiwa wangali wameketi.
Mzozo huo ulizua tofauti nyingi baina ya wazee wa
kanisa na jamaa ya Rapong,o kiasi cha kuwasilishwa kotini ambapo koti iliamuru
kuwa ,marehemu azikwe akiwa ameketi chini.
1 comment:
Waa!! maajabu ya Bungoma kweli
Post a Comment