Wednesday, 30 March 2016

SIMBA AUAWA ISINYA BAADA YA KUTOROKA MBUGA YA WANYAMA

Maafisa wa KWS walilazimika kumpiga risasi baada ya kuwa tishio kwa wakaazi

 Ben Kirui

Simba mmoja aliyetoroka mbuga ya taifa ya wanyamapori ya Nairobi amepigwa risasi na kuuawa na maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori baada ya kumshambulia na kumjeruhi mtu mmoja.
Mapema leo asubuhi simba huyo alitoroka mbuga ya wanyama na kuingia katika maeneo ya makazi karibu na kituo cha kibiashara cha Isinya.
Msemaji wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Paul Gathitu amesema kwamba maafisa walilazimika kumpiga risasi mnyama huyo kwa sababu alikuwa anatishia usalama wa watu.
Amesema maafisa hao walikuwa wametumwa wakiwa na nia ya kumdhibiti lakini akawa mkali zaidi.
Ni kisa ambacho kinatokea siku chache tu baada ya simba mwingine kutoka mbugani na kumjeruhi mtu mmoja katika eneo la Cabanas hapa jijini Nairobi.

No comments: