![]() |
Chumba maalum cha watoto |
By: Joan Kinyua.
Akina mama wenye watoto wachanga nchini Kenya wataweza kwenda kazini na wanao. Hii ni baada ya bunge kupitisha mswada wa Afya ambao utalazimu kampuni kutenga maeneo maalum ya kuwanyonyeshea watoto.
Maeneo hayo maalum
yatakuwa na mashini ya kukamua maziwa ya mama, jokovu la kuhifadhi maziwa na
chakula cha watoto pamoja na kuhakikisha mandhari sawa ya watoto wachanga. Chini
ya mswada huu waajiri lazima watoe muda kwa wanawake kuwanyonyesha watoto hao,
kwa kupokezana.
Rachel Nyamai, mbunge
aliyewasilisha mswada huo amesema utasaidia wanawake kufanya kazi vyema na
wakati huohuo kuimarisha afya ya mtoto. Kwa sasa ni mashirika machache sana
nchini Kenya yanayotenga maeneo maalum ya wanawake kuwanyonyesha wanao.
Hii imewalazimu wanawake wengi kuwacha kuwanyonyesha watoto wao mapema kutokana na masharti na majira ya kazi. Pendekezo sawa na hili lilitupwa nje na bunge lililopita baada ya tume ya waajiri kulalamika na kutishia kuwanyima kazi wanawake.
Mswada wa sasa wa Afya 2015 utawasilishwa kwa bunge ili kuidhinishwa kuwa sheria.
No comments:
Post a Comment