![]() |
Oliver Kilonzo. |
Na Brian Nyaberi.
Mlinzi wa klabu ya Wazito Oliver Kilonzo ameeleza
furaha yake kwa kufaulu kurejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa kpindi cha miezi
mitano kutokana na jeraha.
Beki huyo alicheza katika kipindi cha pili kwenye
mchuano wao na Nakuru All-stars mnamo siku ya Jumapili iliyoisha kwa sare ya
bao 1-1 huku akieleza Imani yake kwamba wameimarika kama timu baada yao
kutoshindwa katika mechi zao nne zilizopita.
Kurejea kwake kutaipiga jeki safu ya ulinzi ya klabu
hiyo ambayo hadi sasa haijafungwa mara moja pekee katika mechi zao kumi za ligi
ya daraja la kwanza ya NSL zilizopita.
No comments:
Post a Comment