Tuesday, 25 October 2016

OKUMBI AKITAJA KIKOSI CHA KENYA.

Wachezaji wa Kenya wakiwa kwenye mazoezi.
Na Mwangi Robert.

Kocha wa Harambee Stars Stanley Okumbi amekitaja kikosi cha wachezaji 25 wanaokipiga kwenye ligi ya nyumbani ili kujiandaa kwa mechi za kirafiki ambazo timu hiyo imeratibiwa kushiriki.
Vijana wa Kenya wameratibiwa kuwa wenyeji kwa timu ya Mozambique na Liberia mnamo tarehe 12 na 15 mtawalia mwezi ujao wa Novemba.
Kando na mastaa wanaocheza katika ligi kuu ya Kenya Okumbi aidha amewaorodhesha wachezaji wanaokipiga kwenye ligi ya daraja la kwanza akiwemo mlinzi wa Vihiga United Bernard Ochieng’ na mwenzake Michael Misigo, kiungo wa Nzoia Sugar Lawrence Juma  na Morven Otinya wa Palos FC.

Stars wanajiandaa kwa Dimba la CECAFA Senior Challenge CUP litakaloandaliwa nchini Kenya.

No comments: