Monday, 24 October 2016

ZOUMA AREJEA UWANJANI BAADA YA KIPINDI KIREFU MKEKANI.

Mchezaji wa Chelsea Kurt Zouma.

Na VIVIAN ATIENO

Baada ya mchezaji wa Chelsea Kurt Zouma kuwa mkekani kwa kipindi cha miezi minane sasa mchezaji huyo ameponya jeraha lake huku akiorodheshwa kwenye kikosi chao cha chipukizi kilichocheza hapo jana.

Zouma alikuwa amepata jeraha la goti katika sare ya bao 1-1 ya ligi kuu nchini uingereza dhidi ya Manchester United.

Kimekuwa kipindi kigumu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amelazimika kuwatazama wenzake wakicheza huku jeraha hilo likimnyima nafasi ya kuliwakilisha taifa lake kwenye michuano ya yuro iliyochezwa nyumbani kwao Ufaransa.


Lakini Zouma alikuwa amefaulu kurejea mazoezini kabla ya msimu huu kung’oa nanga na kupata nafasi ya kufanya mazoezi chini ya meneja wake mpya Antonio Conte.

No comments: