![]() |
Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandag'o |
Ben Kirui
Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago
ameapa kushikilia msimamo wake kuhusu usimamizi wa chuo kikuu cha Moi licha ya
kufika katika makao makuu ya CID kuhojiwa.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya waziri
wa Usalama Joseph Nkaissery kutoa onyo dhidi ya magavana wawili na wabunge kutoka
eneo la North Rift.
Hata hivyo baada ya masaa matatu ya
mahojiano na maafisa wa ujasusi viongozi hao walisisitiza kuwa lazima uteuzi wa
usimamizi wa shule ufanywe kwa njia ya haki huku gavana Mandago alielekezea kidole
cha lawama vyombo vya habari kwa kueneza habari zisizo za ukweli.
Wakati huo huo wenyeji kutoka eneo la
Eldoret waliandamana kupinga kuhojiwa kwa gavana Mandag’o.
No comments:
Post a Comment