Monday, 5 September 2016

MZOZO BAADA YA PAPA KUDAIWA KUMTOROSHA MWANAMKE ANAYEMPOTOSHA.

Papa wa kanisa la Legio Maria.
Mwangi K. Githinji.

Kizaaza kilizuka wakati ambapo kundi la wafuasi wa kanisa la Legio Maria linalomuunga mkono kiongozi wa kanisa hilo liliwafukuza waumini wanaomtuhumu kwa kuwa na ufisadi katika kaunti ya Migori.

Waumini hao waliwafukuza kadinali wanaotuhumiwa na kiongozi huyo kueneza uongo kwamba alitoroka na mwanamke mwenye umri mdogo ambaye anampotosha kuendeleza miradi ya kanisa bila ushauri wa kamati ya kanisa hilo.

Suala hilo limesababisha mgawanyiko baina ya kadinali hao na baadhi ya wafuasi ambao wamemtetea mwanamke huyo kwa kumjengea Nyumba kiongozi huyo anayefahamika kama Papa Romanus Ong’ombe.

No comments: