Friday, 29 January 2016

RAIS KENYATTA AHUDHURIA MKUTANO WA AU ADDIS ABABA

Rais Kenyatta akiondoka nchini
BEN KIRUI

Rais Uhuru Kenyatta ameondoka nchini leo kuelekea Addis Ababa Ethiopia ambako anahudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za umoja wa Afrika.
Katika kikao cha kwanza cha muungano huo Rais Uhuru amewataka marais na viongozi wa mataifa hayo kufanyia marekebisho mfumo wa utendakazi ili kuimarisha mfumo huo
Mkutano huo wa marais wa mataifa wanachama wa (AU) Jumamosi unatarajiwa kuidhinisha ripoti ambayo inapendekeza kujiondoa kwa mataifa ya Afrika kutoka mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Tayari baraza kuu la AU limeidhinisha pendekezo hilo marais wanaokongamana huko Ethiopia sasa wakisubiriwa kuidhinisha ombi hilo jumamosi.
Miongoni mwa masuala mengine yatakayo angaziwa ni pamoja na mkakati wa kupambana na ugaidi.
Uhusiano kati ya ICC na Afrika umezorota kutokana na kesi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto na mwanahabari Joshua Arap Sang’ na amri ya kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir.

No comments: