![]() |
| Tom Wolf mkuu wa utafiti wa IPSOS SYNOVATE |
Ben Kirui
Asilimia 35 ya wakenya wanamtaka kiongozi wa upinzani Raila Odinga astaafu
kabisa kutoka kwenye siasa huku asilimia nyingine 34 ya wakenya wakitaka Raila
asalie kwenye siasa na hata awanie urais mwaka ujao.
Haya ni kwa mujibu wa kura ya maoni uliofanywa na kampuni ya IPSOS mwezi
juni mwaka huu ambapo watu 2,067 kattika kaunti 41 walihojiwa.
Aidha asilimia
25 wana imani na Raila huku asilimia 12 wakiwa na imani na kinara mwenza Moses
Wetangula naye Kalonzo Musyoka akiaminiwa na asilimia 11 tu ya wakenya.
Utafiti huo
pia umearifu kuwa rais Uhuru Kenyatta yuko katika nafasi nzuri ya kukabiliana
na ukabila kwa asilimia 38 huku raila akifuata kwa karibu na asilimia 28.

No comments:
Post a Comment