Tuesday, 26 July 2016

BAADA YA HARAMBEE STARS SASA NI CHIPUKIZI ,KENYA HAINA CHAKE!

Vijana wa Kenya chini ya umri wa miaka 17.
Na Mwangi K. Githinji.

Mchezaji wa Malawi alifunga magoli matatu na hivyo kuwasaidia mababe hao kuicharaza timu ya Kenya chini ya umri wa miaka 17 katika mechi ya michuano ya COSAFAiliyochezwa hapo jana.
 Licha ya  dimba hilo kumalizika bao 1-0 katika kipindi cha kwanza vijana wa Kenya walishindwa kubadilisha matokeo hayo ijapokuwa walifanya mabadiliko kadhaa huku mchezo huo ukiishia mabao 5-0.

Kenya walifungwa mabao kumi kwenye mechi tatu walizocheza ndani ya dimba hilo ambapo walianza kwa kupoteza 4-0 dhidi ya Zambia na kisha baadaye mabao 2-1 walipokabiliana na Madagascar.

No comments: