Ben Kirui
Polisi mjini Nakuru wanamsaka kahaba
mmoja anayedaiwa kuiba bastola ya mlinzi wa gavana wa Turkana Josphat Nanok
bastola iliyopotea mwishoni mwa juma mjini Nakuru.
Akithibitisha
kisa hicho Ocpd wa Nakuru Joshua Nkanatha amesema kuwa mlinzi huyo Benjamin
Lorum ambaye ni afisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Lodwar aliipoteza
bastola hiyo iliyokuwa na risasi kumi na tano pamoja na shillingi elfu 14 baada
ya kuwa na kahaba huyo katika danguro moja mjini Nakuru.
Nkanatha
amesema mlinzi huyo alikuwa ameandamana na gavana Nanok hadi Nairobi kwa
shughuli rasmi za kikazi kabla ya kuomba siku ya mapumziko ijumaa na kuelekea
Nakuru.
Lorum
alipatikana bila nguo wala viatu na akiwa amepoteza fahamu huku kahaba akiwa
ametoweka.
No comments:
Post a Comment