![]() |
| Mawakili na wananchi wakifanya maandamano mjini Nairobi |
Na Ben Kirui
Polisi wanne wa utawala wameshtakiwa
kwa mauwaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake Josphat Mwenda na dereva wa
teksi Joseph Muiruri.
Maafisa hao
wa Ap Fredrick Leliman, Leonard Mwangi, Silvia wanjiku na Stephen Cheburet hata
hivyo wamekana mashtaka mbele ya jaji Jessie Lessit katika mahakama za milimani
hapa jijini Nairobi.
Jaji Lessit
ameamuru wanne hao wazuiliwe rumande kwa siku 30 wakisubiri mahakama kuamua
ombi lao la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.
Kikosi cha
majasusi kutoka humu nchini na marekani Kinaamini kuwa wanne hawa walihusika
katika mauaji ya Kimani na wenzake katika eneo moja karibu na kambi ya polisi
wa utawala ya Syokimau baada ya kukamatwa na kuzuiliwa katika kambi hiyo mwezi
uliopita.

No comments:
Post a Comment