Tuesday, 12 July 2016

WILLIAN ASAINI MKATABA MPYA NA CHELSEA.

Mbrazili Willian.
Na Mwangi K. Githinji
Kiungo wa Brazil Willian amesaini mkataba mpya wa miaka minne utakaombakiza ugani Stamford Bridge hadi mwaka wa 2020.

Tayari the Blues wamemsajili mchezaji Michy Batshuayi na nyongeza hiyo ya mkataba itakuwa ni afueni kwa mkufunzi mpya Antonio Conte ambaye amechukua hatamu klabuni Chelsea hivi majuzi.
Willian alikuwa mchezaji bora wa klabu hicho msimu jana licha yao kusajili msururu wa matokeo mabaya ligini kuu uingereza.

Ilikuwa inakisiwa kuwa nyota huyo angehama Chelsea huku tetesi zikimhusisha na kughuria Manchester United.

Ameeleza furaha yake baada ya kusaini kandarasi na timu hiyo aliyojiunga nayo miaka mitatu iliyopita  akisema kuwa anapania kuendelea kuisaidia kushinda mataji mengi zaidi.

No comments: