![]() |
| Mchezaji Graziano Pelle. |
Na Mwangi K. Githinji.
Mababe wa ligi kuu nchini
uingereza Southampton wameendelea kuwapoteza
wachezaji wao nyota baada ya habari kuibuka kuwa muitalia Graziano Pelle alimejiunga
na klabu cha Uchina Shandong Luneng.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na ‘the Saints’ akitokea Feyenoord mnamo mwaka wa 2014 ambapo aliwachezea mara 81 na kuwafungia mabao 31.
Pelle amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na ataunngana na mchezaji wa Newcastle United Papiss Cisse aliyehamia klabu hicho wiki jana.
Tayari wamewapoteza mastaa Victor Wanyama kwa Tottenham na Sadio Mane aliyeghuria Liverpool.

No comments:
Post a Comment