![]() |
| Maelfu ya watu nchini Sudan Kusini wametoroka makwao |
Ben Kirui
Hali nchini Sudan Kusini inazidi
kudorora huku maelfu ya watu wakiripotiwa kutoroka makwao kutokana na kuendelea
kwa vita.
Jamii ya
kimataifa kipitia kwa shirika la IGAD imeapa kwamba haitaruhusu mapigano
kuendelea katika taifa hilo changa zaidi barani Afrika.
Wakenya walioko
nchini humo wanahofia maisha yao huku wakitaka serikali ya Kenya kuingilia kati
kuwaokoa kwani wanajeshi wameanza kushambulia raia.
Nchi ya
Uganda imelazimika kufunga mpaka wake na Sudan Kusini. Msemaji wa jeshi la Uganda
amesema Uganda imeamua kuchukua hatua hiyo ili kujiweka tayari kuwanasa wale ambao
huenda wakachukua fursa ya hali tete nchini Sudan Kusini kuvuruga amani nchini
Uganda.

No comments:
Post a Comment