Sunday, 10 July 2016

LO! URENO YAMNYIMA MWENYEJI UFARANSA HESHIMA ZAKE.

Wachezaji wa ureno washerehekea ushindi wao dhidi ya Ufaransa.
Na Mwangi K.Githinji.

Timu ya Ureno ililitwaa kombe la mashindano ya yuro yaliyokuwa yakiendelea nchini ufaransa kwa kuwabandua wenyeji hao kwa bao 1-0.
Ureno walicheza bila mchezaji wao nyota na nahodha Christiano Ronaldo ambaye alitolewa nje kunako dakika ya 25 tu ya mcezo kutokana na jeraha la goti.

Licha ya kuondoka uwanjani kwa uchungu mwingi huku akidondokwa na machozi wenzake walitia bidii za mchwa kuhakikisha nyota ya taifa lao inang'aa.

Timu hizo mbili zilitoshana nguvu kwenye muda wa kawaida lakini katika dakika za nyongeza nguvu mpya Eder akafunga bao la kwanza na la mwisho na hivyo kuipa nchi hiyo taji lao la kwanza la mashindano makubwa huko yuropa.

No comments: