Tuesday, 26 April 2016

MAANDAMANO YA UPINZANI KISUMU YATIBUKA

Gavana wa Kisumu Jack Ranguma na wafuasi wa Cord baada ya kutimuliwa na polisi
Ben Kirui

Wafuasi wa upinzani wakiongozwa na gavana wa Kisumu Jack Ranguma wamefurushwa na polisi asubuhi ya leo walipokuwa wakiandamana kuelekea katika afisi za IEBC za kaunti ya Kisumu kwa nia ya kuwafurusha makamishna wa tume hiyo.

Shughuli za biashara zilikwama katika mji wa Kisumu wakati wa maandamano hayo huku polisi wakilazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya wafuasi hao.

Gavana Ranguma amesema alikuwa anawasilisha nia ya mazungumzo ya kutaka kutolewa kwa maafisa wa IEBC.


Ranguma ameshtumu hatua hiyo akisema haitawazuia kuendelea na maandamano ambayo ni halali.

No comments: