![]() |
| Naibu Chansela wa Chuo cha Nairobi Prof Peter Mbithi akihutubiwa wanahabari |
Ben Kirui
Wanafunzi 33 akiwemo
mpinzani mkuu wa Babu Owino Mike Jacobs, wametimuliwa kutoka chuo kikuu cha Nairobi
kwa kushiriki katika maandamano ya hivi majuzi.
Naibu chansela wa chuo hicho profesa Peter Mbithi amesema wanafunzi
wengine 25 wametumwa nyumbani huku wengine 143 wakionywa kwa kushiriki vurugu
hizo.
Hata hivyo usimamizi wa chuo hicho umewapa msamaha wanafunzi wengine 17
waliotuhumiwa kushiriki katika machafuko hayo.
Wakati huo huo Mbithi amesema wataangazia katiba ya muungano wa
wanafunzi wa chuo hicho SONU ili kuzuia vurugu katika siku za baadaye.
Wanafunzi hao walishiriki maandamano kulalamikia uchaguzi wa babu Owino kama
mwenyekiti wa muungano wa wanafunzi SONU.
Chuo hicho kimetangaza rasmi kufunguliwa tena kwa mabewa yake Jumatatu wiki ijayo baada ya kufungwa kwa muda usiojulikana mapema mwezi huu.

No comments:
Post a Comment