![]() |
| Vinara wa Cord Kalonzo Musyoka, Raila Odinga na Moses Wetangula |
Ben Kirui
Muungano wa Cord umewataka wananchi kusahau fedha zilizotokana na mkopo wa Eurobond wakidai ni rasmi kwamba fedha hizo zimepotea.
Wakihutubia wanahabari hapa jijini Nairobi vinara wa muungano huo Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wamewataka wananchi kutotarajia kupata fedha hizo ambazo wanadai zimepotea.
Vinara hao wamefikia hatima hiyo baada ya gavana wa Benki Kuu Dkt Patrick Njoroge kukatalia mbali ombi la Raila Odinga kukutana naye kujadili matumizi ya fedha hizo.

No comments:
Post a Comment