Ben Kirui
Mchungaji wa
kanisa la ACK Mbiruri kaunti ya Embu amefikishwa mahakamani hii leo kujibu
mashtaka ya kumnajisi mpwa wake mwenye umri wa miaka saba.
Mchungaji
huyo Elijah Gichangi hata hivyo, amekana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu wa
mahakama ya Embu Robinson Oigara na akaachiliwa kwa dhamana ya shillingi
100,000.
Hiyo jana
mchungaji huyo alinusurika kifo baada ya wenyeji waliokuwa na ghadhabu kuvamia
hospitali ya Embu level 5 ambako alikuwa amepelekwa na maafisa wa polisi
kufanyiwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment