Monday, 8 February 2016

CHUO CHA CHUKA CHAFUNGWA KUFUATIA GHASIA ZA WANAFUNZI


Wanafunzi wa chuo cha Chuka wakiondoka shuleni

 BEN KIRUI

Chuo kikuu cha Chuka kimefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuzua fujo na kuteketeza basi la chuo hicho na pia kuvunja vioo vya majumba mbalimbali.
Wanafunzi hao wanazozana kuhusiana na uchaguzi wa wawakilishi wa wanafunzi uliofanyika hivi maajuzi ambao sasa umechukua mwelekeo wa ukabila.
Naibu chancellor wa chuo hicho Profesa Erustus Njoka akitangaza kufungwa kwa chuo hicho amesema kuwa uchunguzi kuhusu jinsi uchaguzi ulivyofanya.
Tayari wanafunzi kumi na nane wametiwa nguvuni.

No comments: