Wednesday, 10 February 2016

MAAFISA WAWILI WAPATIKANA NA HATIA YA MAUWAJI


Kwekwe Mwandaza aliyeuawa na polisi Agosti mwaka wa 2014

Ben Kirui

Maafisa 2 wa polisi wanaotuhumiwa kumpiga risasi na kumuua msichana mwenye umri wa miaka 18 wamepatikana na hatia.
Jaji wa mahakama ya Mombasa Martin Muya anasema ushahidi uliowasilishwa umedhibitisha wawili hao Veronica Gitahi na Issa Mzee walihusika na kifo cha Kwekwe Mwandaza mwezi agosti mwaka wa 2014.
Hata hivyo wawili hao wanasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu kifungo chao baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma itakapokamilisha uchunguzo wake.Mahakama pia imefutilia mbali dhamana ya shilingi 500,000 kwa wawili hao na kuwa watazuiliwa katika kituo cha polisi cha bandari.

No comments: