Tuesday, 28 June 2016

MANE AHAMIA LIVERPOOL.

Nyota Sadio Mane.
Na Mwangi K. Githinji.

Miamba wa uingereza  Liverpool  wamemtwaa nyota wa Southampton Sadio Mane kwa kandarasi ya miaka mitano.
Bado kitita walichotumia kumnasa hakijafichuliwa  japo inakisiwa kuwa wamemnunua kwa ada ya yuro milioni 34.

Mane sasa ni mchezaji wa tano kuhama Southampton kuelekea Anfield chini ya kipindi cha miaka miwili baada ya Dejan Lovren, Adam Lallana ,Nathaniel Clyne na Rickie Lambert kufanya hivyo.

No comments: