Tuesday, 7 June 2016

PSG KUMTEMA KOCHA BLANC

Kocha wa PSG Laurent Blanc

Mwangi k Githinji
Klabu cha Paris Saint-Germain kiko tayari kumuachisha kazi mkufunzi Laurent Blanc na kumteua Unai Emery wa Sevilla.
Mababe hao wa Ufaransa walikuwa wanaangazia uwezekano wa kumuajiri Diego Simeone lakini akadinda kuondoka Athletico Madrid.

Hivyo basi sasa wanasaka sahihi ya Emery aliyemaliza msimu huu kwa kutwaa kombe la Yuropa kwa mara ya tatu mtawalia na kukisaidia klabu hicho kumaliza kwenye nafasi ya saba ligini.

Klabu cha PSG kinanuia kushinda taji la klabu bingwa ulaya jambo ambalo Blanc ameshindwa kufanya na kina imani kuwa uteuzi wa Emery utawawezesha kutamba katika michuano ya UEFA.

No comments: